0
Rais JOHN MAGUFULI amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa ZANZIBAR na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMED SHEIN Ikulu Jijini DSM
Rais Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein Ikulu jijini Dar es salaam
Rais JOHN MAGUFULI  amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa ZANZIBAR na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dakta ALI MOHAMED SHEIN Ikulu Jijini DSM.

Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo hayo, Dakta SHEIN amesema  kuwa lengo la mazungumzo hayo ni kumpa taarifa Rais MAGUFULI juu ya hali ya mazungumzo ya kisiasa yanayoendelea huko ZANZIBAR baada ya uchaguzi Mkuu.

Rais SHEIN amesema kuwa  mazungumzo juu ya hali ya ZANZIBAR yaliyoanza tarehe 9 mwezi Novemba mwaka huu  na yanaendelea vizuri chini ya Kamati Maalum ambayo yeye ndiye Mwenyekiti.

Wajumbe wengine wa Kamati Maalum ya mazungumzo juu ya hali ya ZANZIBAR ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa ZANZIBAR, - MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, Makamu wa Pili wa Rais wa ZANZIBAR, - Balozi SEIF ALI IDD  na Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungono wa TANZANIA, -  ALI HASSAN MWINYI.

Wengine ni Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA,  Dakta JAKAYA KIKWETE, Rais Mstaafu wa awamu Sita wa ZANZIBAR Dakta AMANI ABEID KARUME na Rais  Mstaafu wa awamu ya Tano wa ZANZIBAR, Dakta SALMIN AMOUR

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top