0WAZIRI wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk.Diwani Msemo ili kupisha uchunguzi pamoja na mambo mengine ili kubaini  mgongano wa kimaslahi ulioathiri utendaji wa taasisi  hiyo chini ya kaimu mkurugenzi huyo.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto mwenye Wizara hiyo, Ummy Mwalimu imesema kuwa kutokana na ziara alizofanya Rais Dk. John Pombe Magufuli inaonyesha kukosekana kwa dawa katika hospitali za Serikali huku vituo vya afya vya  binafsi vikiwa na dawa.Taarifa ya Waziri huyo imesema kuwa upungufu wa dawa umeendelea kujitokeza kwa karibu zaidi na baadhi ya wagonjwa walieleza kwa uchungu jinsi wanavyopata dawa kwa tabu hatazile wanazotakiwa wapate kwa bei ya ruzuku au zilezinazotakiwa kutolewa bure na serikali.Kwa msingi wa uwazi na uwajibikaji ameagiza watendaji wote wa sekta ya afya hususani wakuu wa vituo vya kutolea huduma za afya, Wafamasia, Wauguzi na Waganga Wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya kukiri kwa maandishi kwa ngazi zao za uwajibikaji endapo wanamiliki Hospitali, Zahanati, Kiliniki, Maduka ya Dawa ndani ya siku 21 kuanzia leo Desemba 23 mwaka huu ambapo  agizo hilo limeotolewa.Aidha taarifa hiyo imedai kuwa kufanya hivyo kutaziba mianya ya upotevu wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya umma.Bodi ya Taasisi ya Ocean Road imeagizwa kutafuta mtu atakayekaimu nafasi iliyoachwa wazi na Dk.Msemo anayefanyiwa uchunguzi.

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top