0


Bomoabomoa bonde la Msimbazi imeanza tayari na baadhi ya nyumba tayari zimeshabomolewa katika eneo la Hananasifu, Kinondoni.

Charles Mkalawa ambaye ni Afisa mipango miji Wizara ya Ardhi alikuwa eneo la tukio na kuzungumza na millardayo.com kuhusu bomoabomoa inayoendelea katika baadhi ya meneo.

Wananchi hawkauwa na taarifa na bomoabomoa..“Serikali inabidi itambue hii hadithi ya kuwatafutia watu fidia inatakiwa ifikie tamati, ilikuwa mwaka juzi, mwaka jana na sasa inaendelea, ifikie hatua watu wafuate sheria, wananchi wengi wamelalamika kuwa hawajapewa taarifa lakini si kweli..tuliwasiliana na viongozi wa Serikali za Mitaa, tumeanza kazi bila uvamizi kutekeleza agizo la Serikali“…

“Kama Wizara si jukumu letu kuwapa wananchi taarifa bali ni viongozi wao wanapaswa kuwapa, wananchi wanaoishi katika maeneo haya hawana uhalali na wanaishi kinyume cha sheria na hakuna uthibitisho wa kukaa hapa, hatuwaonei kwa kuwa hawana uwezo bali tunawasaidia kuepuka na mafuriko”.

Wanananchi waliovunjiwa nyumba zao watapewa fidia?“Miaka mitatu iliyopita walipewa taarifa lakini hawakuwa tayari kuondoka, kuhusu fidia wanapewa wale ambao wana uhalali wa umiliki lakini kumpa mtu fidia ambaye hana uhalali si Sheria na Serikali haitambui”..

Chanzo MillardAyo

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top