0
Klabu ya YANGA imevunja mkataba na mchezaji wao wa kimataifa HARUNA NIYONZIMA baada ya mchezaji huyo kushindwa kuripoti klabuni kama inavyotakiwa
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano JERRY MURO
Klabu ya YANGA imevunja mkataba na mchezaji wao wa kimataifa HARUNA NIYONZIMA baada ya mchezaji huyo kushindwa kuripoti klabuni kama inavyotakiwa.

Mapema hivi karibuni YANGA ilimsimamisha mchezaji huyo kiungo wa kimataifa HARUNA NIYONZIMA kutokana na utovu wa nidhamu ambapo walimpa nusu mshahara na kumtaka atoe maelezo kwanini ameshindwa kuripoti mapema klabuni hapo.

Mambo yamekuwa tofauti tena baada uongozi wa klabu ya YANGA kuchukua hatua ya kuvunja mkataba na mchezaji huyo kama alivyobainisha mkuu wa idara ya habari na mawasiliano JERRY MURO.

Pamoja na kuvunja mkataba huo klabu inamtaka mchezaji huyo kulipa fidia ya jumla ya DOLA za KIMAREKANI elfu 71175 kufidia gharama ambazo klabu imezitumia katika kumuongezea mkataba ambao ungeisha 2017.

JERRY MURO anafafanua iwapo kampuni inataka kumsajili itapswa kulipa fedha zote anazo daiwa na club ya YANGA.

Tangu kuanza tena kwa ligi YANGA ikicheza TANGA michezo miwili na Jijini DSM mchezaji huyo hakushiriki.

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top