0
Ben Pol amewataja wasanii watakaokuwepo kwenye albamu yake aliyopanga kuiachia mwaka huu.
Ben Pol
Ni miaka mingi imepita tangu wasanii wa muziki waache kutoa albamu, lakini hivi karibuni kila msanii ameonekana kuwa na shauku ya kutoa albamu yake akiwemo Ben Pol.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Ben Pol alisema, “Album ipo hatua za mwisho tayari kuna nyimbo tisa zimeisha wanamsubiri Mwana FA.”

“Hapa bongo kutakuwa na Baraka, Ngosha (Fid Q) Afrika tuna Nameless, tuna Avril, Banky W wa Nigeria, pamoja na Chidinma kuna wimbo ambao tunafanya naye hajamaliza bado,” aliongeza.
Kwa sasa Ben Pol anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Moyo Mashine’.

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top