0


Serikali ya Tanzania imetakiwa kuliangalia tatizo la magonjwa yasiyoambukiza kama ni tatizo kubwa nchini na kuweka nguvu kubwa katika tafiti , sera na kutoa elimu zitakazorahisisha mapambano ya magonjwa hayo ili waweze kuwanusuru watanzania.

Kauli hiyo imetolewa na Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof Projestine Muganyizi katika mahojiano maalum na East Africa Radio na kuongeza kuwa hapo awali hakukuwa na takwimu sahihi za magonjwa hayo hali iliyochelewesha harakati za kupambana na magonjwa hayo.

Baadhi ya wananchi walikuwa wakihusisha baadhi ya magonjwa hayo na imani za kishirikina hali iliyopelekea vifo visivyokuwa na sababu kwa sasa matatizo haya yanatangazwa sana na yanaeleweka na jamii hivyo ni jukumu la serikali kurahisisha mapambano yake.

Aidha Prof Muganyizi amesema kuwa magonjwa hayo yasiyoambukiza yanaonekana kushika kasi kwa kipindi hiki ukilinganisha na miaka iliyopita hali inayochangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top