0


Kocha Msaidizi na kocha mkuu wa muda wa Simba, Jackson Mayanja, amewatoa hofu wanachama wa timu yake na kusema muda wowote atatua nchini tayari kusimamia zoezi la usajili.

Mayanja, raia wa Uganda, alipewa likizo ya wiki mbili huku akiwa na matatizo ya kifamilia, lakini sasa yameisha na akili yake yote ipo kwenye mipango ya kuisuka upya timu yake. 

Kutoka Uganda, Mayanja alisema anasubiri uongozi wa Simba umtumie tiketi ya ndege ili arudi Tanzania kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu ujao.

“Waliniambia watanitumia tiketi ya ndege ili nirudi Tanzania kuanza maandalizi ya msimu ujao, mpaka sasa (jana) hawajatuma ila nawasubiria wakituma tu nakuja.

“Nafahamu yanayoendelea, kila kitu kwenye ripoti niliwaelekeza maeneo ya kufanyia usajili, hivyo naamini watayafanya yale niliyoyaainisha kwenye ripoti yangu ya msimu mzima,” alisema Mayanja.


Licha ya Mayanja kutoa kauli hiyo, tayari Simba imehusishwa na usajili wa mabeki Salum Kimenya na Nurdin Chona wa Prisons na Rahim Juma wa African Sports.

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top