0
Mashtaka hayo ni pamoja na shtaka namba moja ya kula njama ya kusambaza taarifa ya uchochezi kupitia gazeti la Mawio lililokuwa na kichwa cha habari cha “Machafuko yaja Zanzibar”, shitaka la tano ni kuwatishia watanzania wa visiwani Zanzibar wasijitokeze kwenye uchaguzi mkuu wa marudio uliofanyika Machi 20 bila kuwa na mamlaka yakufanya hivyo.

Mwendesha mashtaka Wakili Salim Msemo ameiambia mahakama hiyo kuwa hoja ya upande wa utetezi ya kutaka mashitaka matatu yaliyobaki kutosikilizwa mahakamani hapo kuwa haina tija kisheria nakuwa mashtaka yote hayo yasikilizwe mahakamani hapo.

Naye wakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala ameendelea kushikilia msimamo wake wakuitaka mahakama hiyo kufutilia mbali makosa hayo kwani mahakama hiyo haina uwezo wakusikiliza, uamuzi wa shauri hilo utatolewa tarehe 11 Julai 2016.

Mhe. Tundu Lissu na wnzake ambao ni ndugu Simon Mkina muhariri wa gazeti la mawiyo, Ismael Mehboob mchapishaji ambao kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa mnamo tarehe 12 na 14 Januari mwaka huu katika maeneo ya Dar es Salaam walichapisha gazeti lenye kichwa cha habari kilichosomeka “Machafuko yaja Zanzibar” katika gazeti la Mawiyo chapisho namba ISSN 1821 696X no.182 la tarehe 14 January 2016.

Baada ya kuachiwa kwa dhamana Mhe. Tundu Lissu amesema kuwa kitendo cha kufikishwa mahakamani kinalenga kuwaziba midomo na kurudisha nyuma vyama vingi na kuongeza kuwa hata iweje wataendelea na mapambano dhidi ya utawala aliyodaikuwa unawanyima haki yao ya msingi.

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top