0
Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB imeahidi kuchangia Dola Milioni 200 sawa na Shilingi BILIONI 433.6 kwenye Mfuko wa Bajeti Kuu ya Serikali
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali kiasi cha shilingi 433.6bn
 
Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB imeahidi kuchangia Dola Milioni 200  sawa na Shilingi BILIONI 433.6 kwenye Mfuko wa Bajeti Kuu ya Serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017.

         Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo anayeshughulikia Utawala na Rasilimali watu Dokta ALBERIC KACOU alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango Dokta PHILIP MPANGO ofisini kwake Jijini DSM.

Amesema TANZANIA ni nchi inayoongoza katika Bara la Afrika kupewa kiasi kikubwa cha fedha kutokana na mipango yake ya maendeleo inayokidhi vigezo na viwango vya taasisi hiyo.

         Akizungumza na ujumbe huo Waziri wa Fedha na Mipango Dokta PHILIP MPANGO ameshukuru uamuzi wa benki hiyo wa kuongeza mchango wake katika Bajeti Kuu ya Serikali kupitia Mfuko Mkuu wa Bajeti.

         Amesema kuwa serikali imedhamiria kutekeleza mipango yake ya ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa yaani -STANDARD GAUGE pamoja na kununua Ndege TATU za abiria ili kuboresha usafiri wa anga vilevile kununua meli mpya itakayo toa huduma Ziwa Viktoria na kukarabati meli nyingine mbili ambapo moja iko Ziwa Tanganyika na nyingine Ziwa Viktoria ili kuimarisha usafiri wa majini.

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top