0
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa – NDC Dakta CHRISANT MZINDAKAYA amesema kuwa TANZANIA kuwa nchi ya viwanda
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa – NDC Dakta CHRISANT MZINDAKAYA
 
 amesema kuwa TANZANIA kuwa nchi ya viwanda inawezekana endapo watanzania watashiriki kikamilifu katika kuunga mkono serikali katika kufanikisha azma hiyo.

Dakta MZINDAKAYA ametoa kauli hiyo Jijini DSM wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari na kuongeza kuwa ili nchi ipige hatua zaidi kiuchumi ni lazima kuwepo na matumizi bora ya ardhi pamoja na uwezeshaji wa vijana kiuchumi.

Dakta MZINDAKAYA pia amesema kuwa anatarajia kuachia nafasi ya uwenyekiti wa bodi ya NDC kutokana na umri wake kuwa mkubwa.

Kwa sasa Shirika hilo la Maendeleo la Taifa lipo katika mchakato wa utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimaendeleo ikiwemo ile ya Chuma ya MCHUCHUMA na LIGANGA wa Makaa ya Mawe na kiwanda cha viuatilifu kilichopo KIBAHA mkoani PWANI ambacho ni kikubwa Barani AFRIKA.

Aidha ametoa wito kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum wa Chama Cha Mapinduzi -CCM utakaofanyika tarehe 23 mwezi huu kumpa kura nyingi za ndio Rais JOHN MAGUFULI ili awe Mwenyekiti mpya wa chama hicho.

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top