0

Serikali ya Rwanda imekadhibisha tuhuma za Marekani kuwa inahusika na magendo ya binaadamu.

Mathilde Mukantabana, balozi wa Rwanda nchini Marekani hapo jana aliitaja ripoti hiyo kuwa ya kisiasa ambayo iko kinyume na ukweli wa mambo katika jamii ya Wanyarwanda wenyewe.

 Bi, Mukantabana ameogeza kuwa, serikali ya Kigali ina uwezo kamili wa kuwalinda na kuwapa hifadhi wakimbizi hususan raia wa Burundi.

 Balozi huyo amefafanua kuwa, kuwalinda raia wa Burundi mkabala na kufanya magendo ya binaadamu, ni suala linalopewa kipaumbele na serikali ya Rwanda.

 Katika ripoti yake ya mwaka 2015 iliyotolewa siku ya Alkhamisi, Juni 30 Marekani iliituhumu serikali ya Kigali kwamba inashiriki katika magendo ya binaadamu hususan raia wa Burundi.

 Kadhalika ripoti hiyo iliashiria kwamba Rwanda imekuwa ikiwatumia watoto wadogo wa Kirundi kama askari. Hii si mara ya kwanza kwa serikali ya Rais Paul Kagame kutuhumiwa kuhusika na vitendo vya ukandamizaji wa haki za binaadamu.

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top