0
Waziri mkuu mpya wa Uingereza Bibi Theresa May jana aliingia madarakani rasmi na siku hiyohiyo alitangaza baraza jipya la mawaziri. Aliyekuwa meya wa London Bw. Boris Johnson ambaye aliyekuwa kinara wa kampeni ya Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya ameteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje, ambaye atakabiliwa na changamoto ya kushughulikia uhusiano na Umoja wa Ulaya baada ya Uingereza kujitoa. Bibi Ambder Rudd ameteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani ambaye anatarajiwa kuamua namna ya kurekebisha sera za wakimbizi za nchi hiyo.
Bibi Theresa May amesema atajitahidi kujenga taswira mpya ya Uingereza katika jukwaa la kimataifa, huku akisisitiza umuhimu wa umoja wakati sauti za kujitenga zinasikika Scotland na Ireland Kaskazini.

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top