0
Baraza la Taifa ya Elimu ya Ufundi (NACTE) limewatoa hofu wanafunzi waliokuwa katika vyuo vilivyofutiwa usajili na baraza hilo, na kusema kuwa watahamishiwa katika vyuo vingine.
Mkurugenzi wa Usajili na Ithibati NACTE, Bi. Twilumba Mponzi
Mkurugenzi wa Usajili na Ithibati wa baraza hilo Bi. Twilumba Mponzi ametoa kauli hiyo jana katika kipindi cha Hot Mix kinachorushwa na Eatv, kufuatia hatua yake ya kuvifutia usajili vyuo vitano na kuvipa onyo vyuo 41 ambavyo vilibainika kutokuwa na usajili.
Mkurugenzi alikuwa katika mahojiano maalum kuhusu utaratibu wa usajili na ithibati kwa vyuo mbalimbali vinavyosimamiwa na baraza hilo, ambapo alivitaka vyuo 41 vilivyozuiliwa kudahili kwa muda wa wiki mbili, vikamilishe haraka taratibu za usajili, ili viruhusiwe kuendelea na shughuli zake.
Mponzi amesema wanafunzi katika vyuo hivyo hawastahili kuadhibiwa kwa makosa ya vyuo hivyo ni haki yao kutafutiwa vyuo vingine ili wamalizie masomo yao, na kuongeza kuwa baraza hilo litasimamia mchakato huo wa kuwatafutia vyuo wanafunzi hao.
“Kwa kuwa makosa ni ya vyuo na si ya wanafunzi, tutahakikisha wanafunzi hao wanatafutiwa vyuo vingine, lakini hii ni kwa wanafunzi wenye sifa pekee” Amesema Twilumba.
Kuhusu hatma ya vyeti na taaluma za wahitimu wa vyuo hivyo, Mponzi amesema kufutwa kwa vyuo hivyo hakutaathiri ubora na hadi ya vyeti vya waliokwisha hitimu, lakini ni wahitimu ambao walikuwa na sifa za kupata taaluma husika.
“Kama kuna wanafunzi wamehitimu katika vyuo hivyo, tunachoangalia ni kama walikidhi vigezo vya taaluma husika, kama walikidhi, basi tuzo (vyeti) walizopata ni halali, lakini kama hawakuwa na vigezo basi tuzo zao zitakuwa ni batili” Amesema Mponzi.
Aidha Mponzi ametumia nafasi hiyo kuonya watu wanaoanzisha vyuo na kufanya udahili bila kufuata utaratibu, na kusisitiza kuwa kabla ya mtu yeyote kuanzisha chuo anapaswa kwanza kufika katika baraza hilo ili apewe utaratibu na hatua za kufuata kabla ya kupewa usajili.
Kuhusu matangazo mbalimbali, amesema kuwa baraza hilo halihusiki na matangazo ya vyuo mbalimbali, jukumu lake linaishia kufanya usajili, kutoa ithibati pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara.
Pia amevitaka vyuo ambavyo ithibati yake inakwisha, kuhuisha ithibati zao na kufanya maboresho yanayotakiwa ili kukwepa rungu la kufungiwa.
Mponzi amewataka wanafunzi wanaotafuta vyuo kujiridhisha kwanza kuhusu uhalai wa vyuo wanavyotaka kwenda kwa kuangalia kama chuo husika kina usajili kupitia tovuti ya NACTE.

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top