0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amezindua jengo la Upasuaji kwa wanawake wajawazito katika Hospitali ya Mwananyamala Wilaya ya Kinondoni lililojengwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya GSM Foundation.

Makonda Obstetric Theatre kabla halijabadilishwa jina
Jengo hilo limepewa jina la Makonda Obstetric Theatre kutokana na yeye kuwa muasisi wa jitihada hizo alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kabla ya kuteuliwa na Rais John Pombe Magufuli March 13 Mwaka jana kuwa Mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda
Akiongea katika uzinduzi huo RC Makonda amewapongeza GSM Foundation na kuwataka watanzania waunge mkono jitihada za wawekezaji wanao wekeza ndani ya nchi, na kuwataka wananchi kununua bidhaa za wazawa kwani mwisho wa siku wanairejesha faida kwa wananchi kwa kufanya miradi ya maendeleo kama hiyo, huku akisisitiza suala la ulipaji kodi kwa kila mtanzania serikali yeyote duniani haiwezi kujiendesha bila ya kulipa kodi ndiyo maana Rais Magufuli anasisitiza kulipa kodi, hivyo kila mtanzania ajue anamchango katika maendeleo ya taifa kwa kulipa kodi .
Akitoa Muhtasari wa Mradi Mhandisi kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya GSM Foundation waliodhamini ujenzi huo Hersi Saidi ameeleza kuwa ujenzi huo umegharimu kiasi cha shilingi Milioni 420 na kuna vyumba viwili vya upasuaji, huku akisisitiza kuwa watanzania wawe na moyo wa kujitolea kama walivyofanya wao.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta ameeleza kuwa jengo hilo ni muhimu sana kwani linauwezo wa kuhudumia kinamama kati ya 40 na 50 kwa siku hivyo kati ya wanawake 20 na 30 ufanyiwa upasuaji na kupelekea kuondoa msongamano uliokuwepo awali na kufanya huduma zichelewe, pia utaokoa maisha ya wanawake.

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top