0
Ripoti ya Amnesty International

Kwa mujibu wa shirika la Amnesty International Kenya na Tanzania zimetajwa katika jumla ya nchi za kiafrika ambazo zimekuwa mstari wa mbele kuwakandamiza wapinzani na kunyongesha uhuru wa kujielezea.
Shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International, limesema mwaka 2016/17 uligubikwa na wimbi la uvunjifu wa haki za binadamu.

Pia limeeleza kuwa watetezi wa haki za binadamu na waandishi wa habari, kwa mfululizo, wameendelea kukabiliwa na vitendo vya uvunjifu wa amani.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa haki ya uhuru wa kujielezea ilikabiliwa na mmomonyoko mkubwa pamoja na wimbi jipya la vitisho kutoka katika vyombo vya dola.

Kumekuwa na jaribio la kukandamiza wapinzani na kunyongesha uhuru wa kujielezea vilivyo jitokeza katika bara zima la Afrika, imesema ripoti hiyo.

Nchi nyingine zilizoorodheshwa katika ripoti hiyo na kuhusishwa na uvunjifu huo wa haki za binadamu ni pamoja na Botswana, Burundi, Cameroon, Chad, Côte d’Ivoire, Gambia,Mauritania, Nigeria, Somalia, South Sudan, Sudan, Togo and Zambia.

Ripoti imesema hayo ni kati ya zaidi ya matukio 177 ya watu binafsi waliouwawa kinyume cha sheria, wakati wakiwa mikononi mwa vyombo vya usalama kwa mwaka mzima (2016/17).

Nchi nyingine hizo 14 ziliorodheshwa ni kati ya zile zinazoongoza katika kukandamiza uhuru wa kujielezea na pia ukamataji wa kiholela na kuwaweka kizuizini wanachama wa vyama vya upinzani na makundi mengine.

Katika ripoti hiyo ya Amnesty International matukio mengi yameshuhudiwa katika maeneo ya pwani, na vitendo hivyo vya uvunjaji wa haki za binadamu vimekuwa vikitekelezwa kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na mashambulizi ya kundi la kigaidi la al-Shabaab.

“Kwa mujibu wa Haki Afrika, kikundi cha haki za binadamu, kulikuwa na mauaji 78 kinyume cha sheria na kutoweka kwa watu bila ya taarifa yoyote katika kaunti ya Mombasa katika miezi 8 ya kwanza ya 2016.

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top