0

Lakini yote kwa yote bado changamoto ipo, wanawake tuliowaoa ni mashushushu kupita maelezo, wanataka kujua kila kinachofanyika ndani ya simu zetu. Wanataka kufahamu ulimpigia nani, nani alikutumia meseji na nani ulimfanyia muamala— wanataka kujua kila kitu.
Na hapa wapo wa aina mbili— wapo wale wanaogundua na kukuanzishia varangati wewe muhusika mkuu, na kuna hawa wengine wanaogundua na kuanza kufanya upelelezi bila kukupa taarifa— hawa ndo wabaya zaidi.
Hawa wapelelezi wana kawaida ya kuchukua namba yoyote ambayo anaihisi vibaya, hata kama anachokihisi hakina ukweli. Na anaanza kuifuatilia. Na matokeo yake mara nyingi huchukua namba ambazo hata haziusiani na fikra zake na matokeo yake wanaweza kukupotezea hata ukaribu na watu wako wengine muhimu.
Sasa juzi katika vikao vyetu tulikuwa tunaijadili hii mada, ni jinsi gani unaweza kumzuia mwanamke mwenye tabia ya kuingia kwenye simu yako na kuchukua namba ambazo anahisi zinamilikiwa na watu ambao si salama kwa uhai wa ndoa yake.
Kila mtu akawa anachangia namna ambavyo yeye anajaribu kujitoa kwa hilo tatizo ingawa nusu na robo ya wote wenye matatizo hayo hatujafanikiwa kwa kiasi hicho kwa kutumia hizo njia zetu.
Wengine wakawa wanasema ukumbuke kufuata namba mara tu unapomaliza kufanya mambo yako. Lakini sio kila simu au meseji zinakuja kwa uhuru namna hiyo—matatizo mengine yanatokea ukiwa kwenye mishuhuliko, unachokifanya ni kumalizana nayo haraka haraka unaendelea na kazi yako.
Wengine wakasema basi uwe unajiwekea utaratibu wa kufuata mawasilinao ya siku nzima kabla hujatia miguu yako nyumbani. Lakini hiyo mbona watu wengi tunafanya na bado matatizo yapo palepale.
Mwisho akachangia jamaa yetu mmoja yeye akaja na njia ya kidigitali zaidi. Anakwambia kwenye hizi simu za kisasa hizi kuna programu unaweza kuipakua inaitwa Calcont— ni calculator lakini inafanya kazi ya ziada ya kuficha namba zako zote ambazo unataka ziwe siri.
Jamaa anakwambia kwa muonekano hiyo programu ni kama calculator kabisa na ina uwezo hata wa kufanya hesabu na mambo yote ambayo calculator hufanya. Lakini nyuma ya pazia, programu hii inaweza kuhifadhi namba za simu ambazo hazitaonekana sehemu nyingine yeyote kwenye simu yako (hata kwenye ‘phonebook’ ya kawaida) hivyo ni wewe tu ambaye utakuwa na uwezo wa kuziona kwa sababu ili uzifikie, ni lazima ufanye hesabu ambayo inakuwa kama neno la siri, ambayo hesabu hiyi unaichagua pindi unapo-install progaramu kwenye simu yako.
Kwa mfano, unaweza kuweka moja kumjulisha moja, na ukibofya alama ya sawasawa, badala ya kukupa jibu la swali hilo itakupelekea mahala ambapo namba za watu wako wa siri umezificha. Huko unaweza kufanya mawasiliano na namba hizo kwa kuzipigia simu, kuzitumia meseji za kawaida na meseji za WhatsApp.
Halafu jamaa anakwambia, hiyo programu ukimaliza kuzungumza tu au kutuma meseji inakukumbusha kufuta hapohapo. Kwahiyo haikupi kabisa fursa ya kujisahau.
Hadi jamaa anamaliza kutupa somo kila mmoja alikuwa tayari na hiyo kitu kwenye smu yake.
Kwa nini tupate tabu wakati tunaishi kwenye dunia iliyorahisihwa bwana.
Anaandika Mwananchi Communication


Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top