0
Waziri wa maji na umwagiliaji  Mhandisi Isack Kamwelwe amekabidhi kiasi cha shilingi milioni 20 kwa ajili ya mradi wa maji  katika mtaa wa Bukala kata ya Ibisabageni  wilayani Sengerema mkoani Mwanza. 
  
Akizungumza katika mkutano wa wananchi na viongozi wakati akikabidhi mabomba hayo , katika mtaa wa Bukala  waziri kamwelwe amesema kuwa wananchi washirikiane pamoja na viongozi ili kuweza kupata maji safi na salaama na kutoa agizo kuwa  ndani ya wiki tatu maji yawe yamepatikana

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Sengerema  mh.Emmanuel Kipole amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutumia nguvu kazi ili kuhakikisha zoezi la  upatikanaji wa maji linakamilika mapema ili kuondokana na changamoto hiyo .
  
Mh .kipole ameongeza kwa kusema kuwa wanafanya jitihada za upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali ili kusaidia wananchi na kuunga mkono kauli ya mh. Rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe Dkt .JOHN POMBE MAGUFULI ya kumtua ndoo ya maji mama.

Sambamba na hayo wananchi wa wilaya hiyo wamemshukuru waziri  wa maji na umwagiliaji mhandisi  kamwelwe  na kusema kuwa, tatizo la maji limekuwa likiwasumbua kwa muda mrefu hivyo wamepokea mabomba hayo kwa furaha .

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top