0

Upungufu wa vifaa umepelekea zoezi la upimaji wa  viwanja  kuchelewa katika   mtaa   wa   Kanyamwanza  kata ya Mwabaluhi wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Katibu wa  kamati  ya  upimaji  na  urasimishaji  wa  viwanja   katika mtaa huo  Bwn,Joseph  Maxmiliani  Kayanda ameeleza upimaji  ulivyoanza  mtaani  hapo.

Katibu  huyo  amezungumzia  jitihada  wanazozifanya  kama  kamati  kuhakikisha  kampuni  ya  Geop  Geomatix Interprisess inaongeza   vifaa   ili  kukamilisha upimaji  kwa  wakati.

Aidha Bwn, kayanda amekiri kukumbana na changamoto  katika  zoezi  hilo   ikiwemo  uelewa mdogo wa  wananchi juu ya hatimiliki inayotolewa sasa na Ofa zilizokuwa  zikitolewa  awali.

Hata hivyo  katibu  huyo  amewataka  wananchi  kutambua  umuhimu  wa  hatimiliki   na  kwamba  inaweza  kuwasaidia  katika  mambo mbalimbali  sambamba  na  kuwa  na  uhakika  wa  kumiliki  aridhi  kisheria.Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top