0
Image result for vijana wajasiliamali
Vijana mkoani njombe wametakiwa kuungana kuanzisha vikundi ili kupambana  umasikini pamoja na kukabiliana na changamoto ya ajira.

Akizungumza Jana  na makatibu kata wilaya ya Njombe,Mwenyekiti wa jumuiya ya Vijana CCM Nehemia Tweve,alisema kuwa serikali inampango madhubuti wa kuhakikisha inawakwamua Vijana kutoka katika umasikini kwa kuunda vikundi.

"Hakuna Fedha itakayotolewa kwa mtu mmoja mmoja ni lazima tuzingatie suala la vikundi....unganeni muwe watu hata zaidi ya watano mnatosha kuanza shughuri mnayoitaka kwa ajili ya kujiajiri" alisema Tweve.

Aliongeza kuwa "halmashauri wanatoa asilimia tano ya mapato ya ndani ili kukopeshwa Vijana lakini hamjitokezi badala yake mnalalamika tu kuwa maisha magumu" alisema Tweve.
 
Tweve Alisema Vijana wanatakiwa kujihimarisha kwa kupambana na umasikini kwa vitendo na sio maneno.

"Kwenye kupambana na umasikini ni lazima tuamue kweli maneno matupu hayatu
saidii badala yake tutazidi kuwa masikini" alisema Tweve.

Kwa upande wa katibu wa jumuiya ya Vijana Chama cha mapinduzi Ccm Mkoa wa Njombe, Sure Mwasanguti,aliwataka viongozi wa jumuiya hiyo wilaya ya Njombe kuhakiki Mali za jumuiya hiyo ili kuzijua.

"Jumuiya ionyeshe Mali zote ili tuweze kuzijua,kama kuna mashamba tuyaendeleze kwani Mkoa wetu Kilimo kinakubali hivyo ni wakati sasa wa kuyatumia kwa ajili ya shughuri" alisema Mwasanguti. 

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top