0
Halmashauri ya mji wa Njombe imetoa taswira ya muonekano mpya wa halmashauri hiy baada ya miaka kadhaa ijayo na kuonhyesha maeneo ya  vipamumbele dara ya ardhi imewasilisha mpango wa muonekanano mpya wa nyumba na makazi ambao kwa kiasi kikubwa unalenga kupunguza matumizi ya ardhi .

Kwa kiasi kikubwa mpango huo ambao utatoa fura ya kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji na kilimo huenda ukawa na nafuu zaidi kwa wakazi wa mji huo.

Taarifa hiyo imewasilishwa jana na Afisa Mipango miji Enock Mligo kwa wadau wa kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo za binafsi na za serikali ili kujaribu kuutathimini na kutolea maoni juu ya ubinifu huo.

Lengo kuu la kutengeneza mpango huu kabambe ni Kuwezesha mamlaka  kusimamia ukuaji, kutoa huduma, na kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo,Kuwezesha eneo lenye shughuli za kimji kuwa na matumizi bora ya Ardhi na yenye tija.

Lakini pia inatoa mwanya wa Kuwezesha maisha bora kwa wakazi, kufungua fursa mbalimbali za maendeleo mfano, Ajira, biashara, huduma za viwanda, usafiri na usafirishaji,na fursa nyinginezo nyingi.

Bado kuna hofu ambayo imekuwa ni changamoto kubwa ya wananchi kutokuheshimu utekelezaji wa mipango hiyo ikiwemo ujenzi holela wa nyumba bila mipangilio na kuacha maeneo ya wazi.

Baada ya kuwasilishwa kwa taarifa hiyo wadau mbalimbali wakapata nafasi ya kuichambua na kwa sehemu kubwa licha ya kuonyesha uhalisia wake bado wameitaka timu ya ubunifu kuangalia namna hya kutenga maeneo ya vipaumbele na maeneo mengine kwa ajili ya shughuli muhimu kama vile mazishi.

Wasi wasi mkubwa bado unaoenekana katika eneo la uwekezaji ambalo mara nyingi wawekezaji hufanya shughuli tofauti na vibali vyao vinavyowaelekeza na kuitaka serikali kuwabana wale wote wanaokiuka mashart ya vibali vyao.

Kuhusu sekta ya kilimo wanaonelea kila kata itambuliwe kwa shughuli yake yaani kama ni kilimo na kushauri kutenga maeneo ya huduma muhimu kama shule,matibabu na mambo mengine.

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Mkoa wa Njombe ni mkoa wa pili Tanzania kwa kuwa na idadi kubwa ya watu ikiongozwa na Mkoa wa Dar Es Salaam,hivyo katika mpango huo halmashauri ya mji pekee imebainika kuwa na  Eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 3,212 lenye jumla ya Hekta 321,000
 

Maana ya Mpango Kamambe
Ni mpango wa jumla au Dira inayosimamia ukuaji wa Mji kwa muda mrefu (kawaida miaka 20)
Huonyesha matumizi mbalimbali ya ardhi kwa ujumla wake mfano:
»Maeneo ya viwanda
»Maeneo ya Huduma za kijamii
»Maeneo ya uwekezaji
»Maeneo ya kibiashara
»Maeneo ya Kilimo na ufugaji
»Maeneo ya Hifadhi
»Maeneo ya Makazi nk


 

Post a Comment

(function(i,s,o,g,r,a,m){i['GoogleAnalyticsObject']=r;i[r]=i[r]||function(){ (i[r].q=i[r].q||[]).push(arguments)},i[r].l=1*new Date();a=s.createElement(o), m=s.getElementsByTagName(o)[0];a.async=1;a.src=g;m.parentNode.insertBefore(a,m) })(window,document,'script','https://www.google-analytics.com/analytics.js','ga'); ga('create', 'UA-87191200-1', 'auto'); ga('send', 'pageview'); ga('set', 'userId', {{USER_ID}}); // Set the user ID using signed-in user_id.
 
Top